Pages

Saturday, September 16, 2017

Singida United FC yaja na Singida United TV kupitia Azam tv

Klabu ya Singida United Football Club kupitia kwa Mkurugenzi wake Ndg. Festo Sanga ametangaza habari njema  kwa Klabu hiyo  kwa kuingia  mkataba wa mafanikio na mnono wa miaka mitatu wa kuanzishwa kwa SINGIDA UNITED TV kupitia Azam Tv.
Akizungumza kwa furaha, Mkurugenzi huyo, amesema:  “Tunawashukuru Uhai production wanaoendesha Azam Tv kwa kukubali kuanzishwa kwa kipindi cha Singida United Tv kitakachokuwa kinarushwa kupitia Azam Tv. Ni mafanikio ya kujivunia kuona kila mkakati tunaoupanga unafikia maleng.
Tunaendelea kuwaomba watanzania na wadau wa mpira kuwa tuungane kuleta mabadiliko ya uendeshaji wa vilabu vyetu na zaidi soka kwa ujumla. “Pia kuanzishwa kwa SINGIDA UNITED TV ni moja ya njia ya kuwatangaza wadhamini wetu ambao wamewekeza kwenye club yetu.” Alieleza Sanga.

Mtendaji Mkuu wa Uhai Production,  Ndg. Tido Mhando akimkabidhi mkataba walioingia leo na Singida United, ndg. Festo sanga Mkurugenzi wa Singida United Football Club.

No comments:

Post a Comment