Pages

Monday, September 4, 2017

SIMBA YAUNDA KAMATI YA KUSIMAMIA MCHAKATO WA ZABUNI ZA HISA

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba imeunda Kamati ya watu watano kusimamia mchakato wa zabuni kuwapata wawekezaji ambao ni wanachama wa klabu hiyo watakaonunua asilimia 50 ya hisa zao.

Hatua hiyo imetangazwa jana Dar es Salaam baada ya kamati kukutana kujadili mchakato wa kubadilisha muundo wa uendeshaji kufuatia wanachama 1,200 kupitisha kwenye mkutano wa wanachama uliofanyika Agosti 20, 2017.

Katibu Mkuu wa Simba, Dk Arnold Kashembe alisema kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti, Jaji mstaafu Thomas Mihayo ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini (TTB).

Wajumbe ni Wakili Damas Ndumbaro, Azzan Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala, Abdulrazaq Badru ambaye ni Mkurugenzi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini na Dk Yusuf Majid, mtaalamu wa masuala ya ununuzi nchini.

Mkuu wa Idara ya Habari Simba, Haji Manara alifafanua kuwa katika asilimia 100 za hisa, 50 zinatakiwa ziuzwe kwa mwanachama wa Simba katika mfumo wa tenda na 50 zilizobaki hisa 10 zitakuwa za wanachama na 40 zitakuwa mtaji.

"Kamati haitaingiliwa na mtu kwani itafanya kazi kwa mujibu wa sheria za manunuzi ya umma na za nchi hii na mshindi atatangazwa na jina lake kupelekwa kwa wanachama," alisema.

Manara amewahimiza wanachama wa Simba wenye uwezo wa kununua hisa wajitokeze na kufanya uwekezaji huo kwa manufaa ya klabu.

Katika hatua nyingine, Manara ameiomba Serikali kushirikiana nao kuwakamata watu wanaouza jezi bandia mtaani na  mechi za soka uwanja wa Taifa ili wachukuliwe hatua kali.

"Kama Serikali ilishirikiana na wasanii kudhibiti CD bandia, inaweza kushirikiana na sisi kudhibiti jezi bandia kwa sababu wako wauzaji wengi wanatunyima mapato," alisema.

No comments:

Post a Comment