Pages

Monday, September 4, 2017

SIMBA NA YANGA SASA OCTOBA 28 BADALA YA OCTOBA 14 PIA ZITACHEZA CHAMAZI NA AZAM FC

YANGA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 28 Uwanja wa Uhuru kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotoka leo.
Kwa mujibu wa ratiba ya awali ambayo uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliunda kikosi kazi kwa ajili ya kuipitia kwa sababu ya kuwa na mapungufu mengi, mchezo huo ulikuwa huchezwa Oktoba 14 na Simba ndio alikuwa mwenyeji.
Raundi ya pili zitakutana raundi ya 23 ambayo inataanza Machi 14 lakini haujapangiwa tarehe wakati awali zilikuwa zikutane raundi Machi 3, 2018
Pazia la ligi linatarajiwa kufungwa Mei 26, ambapo Simba itamaliza ugenini kwa kucheza na Majimaji na Yanga itamaza nyumbani kwa kucheza na Azam FC
Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema mchezo wa Simba na Yanga umesogezwa mbele kwa 14 katika raundi ya nane  na dirisha dogo linatarajiwa kufunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15.
“Ratiba imebadilika kwa kiasi kikubwa kwani kwa mujibu wa ratiba ya awali ligi ilikuwa imalizike Mei 5, 2018 lakini sasa itamalizika Mei 28, 2018 siku 21 zaidi,” alisema Lucas.
Pia Lucas alisema raundi ya pili itaanza Januari 19, 2018 badala ya Disemba 30, 2017 kama ratiba ya awali ilivyoonesha. 
Baada ya michezo ya Agosti 26 na 27, Ligi Kuu ya sasa itaendelea Septemba 9 na 10 kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja tofauti.

No comments:

Post a Comment