Pages

Wednesday, September 6, 2017

SERENGETI BOYS KAMBINI WIKI TATU KUJIANDAA NA AFCON 2019





TIMU ya Taifa ya soka ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 15 ‘Serengeti boys’ ipo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Vijana ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini 2019.
Timu hiyo ambayo inaandaliwa kushiriki fainali za U-17 za Afrika 2019 ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji kila mwezi hukaa kambini kwa siku 21 kwa ajili ya kujenga kikosi imara ambacho kitaleta ushindani katika fainali hizo.
Akizungumza Kocha wa timu hiyo Oscar Mirambo alisema waliingia kambini tangu juzi na itachukua siku 21 ili kuwafundisha wachezaji mbinu mbalimbali za soka baadae wapate kikosi imara.
“Hii timu ndio tunaiandaa kwa ajili ya fainali za 2019 ambazo tutakuwa wenyeji na sisi tumejiwekea kawaida ya kukutana kila mwezi kwa wiki mbili,” alisema Mirambo.
“Huu ni mwaka wa mwisho wa kufanya scouting hivyo wachezaji waliopatikana katika mashindano ya Umitashumta na mashindano ya U-12 yaliyofanyika Mwanza miaka mitatu iliyopita ndio tunaendelea kuangalia vipaji ili tubaki na wachezaji wazuri,” alisema Mirambo
Pia Mirambo alisema wachezaji hao wapo vizuri kwani walianza kukaa pamoja zaidi ya miaka miwili hivyo anaamini kitakuwa kikosi kizuri kama ilivyokuwa Serengeti boys iliyopita.
Kitendo cha Tanzania kuwa mwenyeji wa Afcon U-17 inapata nafasi ya kushiriki moja kwa moja hata kama itapata nafasi kwenye makundi.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa timu ya Vijana kushiriki Afcon U-17 baada ya mwaka huu kushiriki fainali za Gabon na kuondolewa kwenye hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment