Pages

Wednesday, September 6, 2017

LIGI YA WANAWAKE KUANZA SEPTEMBA 22-29






LIGI ndogo ya timu za wanawake ya kutafuta timu mbili ambazo zitapanda daraja inatarajiwa kuanza Septemba 22-29 mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari leo
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema Makatibu wa vyama vya  soka la wanawake wa mikoa wameagizwa kupeleka majina ya timubingwa wa mkoa kwa ajili ya kucheza ligi hiyo.


“Viva ya Mtwara na Victoria queens ya Kagera zilishuka daraja baada ya ligi ya wanawake iliyopita hivyo itachezwa ligi kupata timu mbili ambazo zitaungana na timu 10 zilizopo ligi kuu ya wanawake,” alisema Lucas.

Lucas alisema ili kupata timu mbili zitakazopanda daraja ligi hiyo itagawanywa katika makundi mawili hivyo mshindi wa kwanza wa kila kundi ndie atakayepanda
Aidha Lucas alisema wanaendelea kutafuta mfadhili kwa ajili ya ligi hiyo.

Timu ambazo zipo ligi kuu ni bingwa Mlandizi Queens ya Pwani,  JKT Queens, Evergreen, Mburahati Queens za Dar es Salaam, Fair Play ya Tanga, Marsh Academy ya Mwanza, Baobab ya Dodoma, Majengo Women ya Singida, Sisters ya Kigoma, Panama FC

No comments:

Post a Comment