Pages

Friday, August 25, 2017

TFF YAOMBA RADHI





UONGOZI wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), umeomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa juzi

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha Simba na Yanga za Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Simba ilishinda kwa penalti 5-4 na kutwaa Ngao hiyo. 
Ngao hiyo ambayo ilitengenezwa kwa mbao iliandikwa Community Sheild badala ya Community Shield neno ambalo lilipoteza maana ya neno Ngao ya jamii na wadau wengine wakihoji kwanini hawakutumia lugha adhimu ya Kiswahili
Akizungumza na gazeti hili, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Watanzania hususani wanafamilia ya soka TFF haijapokea vizuri muonekana wenye makosa kwenye Ngao ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

“Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika na amewasiliana na uongozi wa Simba kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi,” alisema Lucas

Pia Lucas alisema hawategemei tukio kama hili kujirudia tena.
Hii ni mara ya pili Ngao ya Jamii inayotolewa na TFF kuwa na makosa kwani msimu wa 2016-2017 Azam FC baada ya kuifunga Yanga ilipewa Ngao ambayo ilibanduka maandishi yaliyobandikwa kwani ilikuwa ya kioo.

No comments:

Post a Comment