Pages

Friday, August 25, 2017

NIYONZIMA AMKUBALI TSHISHIMBI


KIUNGO mpya wa Simba Haruna Niyonzima amemwagia sifa Mkongomani wa Yanga Papy Tshishimbi kwa uwezo aliouonyesha katika mechi ya watani wa jadi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Niyonzima raia wa Rwanda amesema Tshishimbi ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi ambayo hutawaliwa na presha kutoka kwa mashabiki na pande zote mbili.
Tshishimbi ambaye ni kiungo mkabaji alicheza dakika zote 90 akiwadhibiti vilivyo viungo wa Simba huku akitumika pia kupandisha mashambulizi kwa kupiga pasi ndefu japokuwa nyingi hazikuwa na madhara kwa Wekundu hao.

“Tshishimbi ameanza vizuri nampongeza, amecheza vizuri katika mechi yenye presha kubwa, kama ataendelea hivi naamini ataisaidia sana Yanga katika safu ya kiungo.“Mpira wa Bongo una mambo mengi sana, kwahiyo ni lazima apate muda auzoee ndipo ataweza kudumu katika kiwango chake hiki na kuwa tegemeo katika timu,” alisema Niyonzima. Kiungo huyo pia amewapongeza mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuwapa moyo kitu ambacho kiliwafanya wachezaji kuona wana deni kubwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
“Mashabiki wetu wamejitokeza kwa wingi na walitupa sapoti kubwa, niwaombe waendelee kuwa pamoja nasi katika ligi ili tufanye vizuri,” alisema Niyonzima.

No comments:

Post a Comment