Pages

Tuesday, August 29, 2017

TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI LEO KUJIWINDA NA BOTSWANA







TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana unaotarajiwa kuchezwa Septemba 2
Elias Maguli ni mchezaji pekee anayecheza soka nje aliyeanza mazoezi huko nahodha Mbwana Samatta akitajwa kuwasili alfajiri na kufanya idadi kuwa 16 huku wengine watano wakitarajiwa kuwasili leo.
Katika mazoezi yaliyofanyika jana kocha Ami Ninje wa Zanzibar ambaye anafanya shughuli zake nchini Uingereza alikuwa miongoni mwa benchi la ufundi linaloongozwa na Salum Mayanga.
Ami alifundisha sehemu ya pili ya mazoezi ya uwanjani baada ya sehemu ya kwanza ya kupashwa mwili joto kufanywa na kocha msaidizi Fulgence Novatus na sehemu ya tatu iliendeshwa na kocha mkuu Salum Mayanga.
Akizungumza kando ya mazoezi hayo, Mayanga alisema baada ya wachezaji kuingia kambini juzi walifanyiwa vipimo vya afya na na kusema wachezaji wanaocheza nje wanatarajiwa kuwasili jana usiku.
“Wachezaji wako fiti ni kama unavyowaona wanafanya mazoezi na morali ipo juu kuikabili Botswana, kesho (leo) natarajiwa wachezaji wanaocheza soka nje watakuwepo,” alisema Mayanga.
Lucas amesema wamekwishafanya mawasiliano na wachezaji wanaocheza nje walioitwa kujiunga na kikosi cha Stars akiwemo Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili ni Farid Mussa, Simon Msuva, Hamisi Abdalla, Ergenes Mollel na Abdi Banda.
Wakati huo huo Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas alisema msafara wa wachezaji 18 na viongozi tisa kutoka Botswana unatarajiwa kuwasili kesho na Ijumaa watafanya mazoezi katika uwanja wa Uhuru
 “Tumewasiliana na Botswana na wamesema watakuja na msafara wa watu 27 ambao ni wachezaji 18 na viongozi tisa,” alisema Lucas.
Mchezo huu ni kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la dunia ambayo huchezwa kila mwezi.

No comments:

Post a Comment