Pages

Wednesday, August 23, 2017

SITA DARAJA LA KWANZA KUPANDA LIGI KUU



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Kamati ya Utendaji, limeongeza idadi ya timu shiriki kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao 2018/19 kutoka 16 hadi 20 ili kuongeza ushindani zaidi katika ligi.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema uamuzi huo umepitishwa jana na Kamati ya Utendaji ya TFF iliyofanyia marekebisho Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayoanza Septemba 16, mwaka huu.

Alisema kutokana na marekebisho hayo, timu zitakazoshuka daraja mwishoni mwa msimu huu kutoka Ligi Kuu ni mbili hivyo kubaki 14 ili kuzifanya nne zitakazopanda ziungane na mbili kufanya ziwe 20.

“Kwa mujibu wa utaratibu wa Ligi Daraja la Kwanza, ina maana msimu huu timu mbili zitapanda kutoka katika kila kundi katika ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu,” alisema Lucas.

No comments:

Post a Comment