Pages

Thursday, August 24, 2017

BARCELONA WAPANDISHA DAU ILI WAMPATE PHILIPPE COUTINHO, CHELSEA NAO WAMPANIA DANNY DRINKWATER NA JAMIE VARDY.


Barcelona watapanda dau la mwisho la pauni milioni 136 kumtaka kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, baada ya dau la kwanza, la pili na la tatu kukataliwa. (Sun)

Barcelona wamepanda dau la pili la pauni milioni 119 kumtaka mshambuliali wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, lakini Dortmund wanataka pauni milioni 138. (Sky Deutschland)

Barcelona wamebadili mawazo ya kumsajili kiungo wa Nice, Jean Michael Seri. (Mundo Deportivo)

Chelsea watamchukua meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel kuziba nafasi ya Antonio Conte, huku taarifa za mvutano kati ya Conte na utawala wa Chelsea zikizidi kurindima. (Bild)

Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa Danny Drinkwater, 27, kutoka Leicester kwa pauni milioni 30. Chelsea pia wanamtaka kiungo wa Inter Milan Antonio Candreva, 30, ambaye ameambiwa atauzwa kwa pauni milioni 25. (Mirror)
Chelsea wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy, 30. (Mirror)
Chelsea bado wanamfuatilia mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti, 23. (Star)
Licha ya kukataliwa mara kadhaa, Chelsea watapanda dau jingine la euro milioni 70 kumtaka beki wa Juventus Alex Sandro. (Calciomercato.com)

Chelsea wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 35 kumtaka kiungo mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka. (The Sun)


Alex Oxlade-Chamberlain, 24, hana uhakika wa kusaini mkataba mpya Emirates, huku Chelsea na Liverpool wakiendelea kumnyatia. (Telegraph)

Paris Saint-Germain watamlipa mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, mshahara wa pauni milioni 13.8 kwa mwaka, mara mbili ya mshahara alioahidiwa kupewa na Real Madrid. (Marca)

Beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose, 27, atakuwa na mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake huku Chelsea na Manchester United wakiendelea kumnyatia. (Independent)


Tottenham wana matumaini ya kumsajili beki wa kulia wa PSG Serge Aurier, 24, pamoja na beki wa Estudiantes Juan Foyth. (Sky Sports)

Manchester City wanajiandaa kupanda dau la pili kumtaka beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 18 kukataliwa wiki iliyopita. (ESPN)

Manchester United wamekuwa namazungumzo na Inter Milan kuhusu uhamisho wa Ivan Perisic, 28, tangu mwisho wa msimu uliopita, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia anatarajiwa kusaini mkataba mpya Inter. (Star)

Manchester United ni miongoni mwa timu zinazomfuatilia beki wa kati wa Valencia Ezequiel Garay. (The Sun)


Manchester United, West Ham, Everton, Monaco na Anerlecht zinamnyatia mshambuliaji Raul Jiminez wa Benfica. (ESPN Mexico)

Everton wamepanda dau la pauni milioni 27.5 kumtaka mshambuliaji wa Benfica Raul Jiminez. (The Sun)

Arsenal huenda wakashawishiwa kumuuza Alexis Sanchez kwa pauni milioni 70, lakini Arsene Wenger amedhamiria kutomuuza. (Daily Mirror)

Marseille wamethibitisha kuwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, iwapo atashindwa kwenda Atletico Madrid. (Telegraph)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kumsajili beki wa Schalke Benedikt Howedes, 29, kwa pauni milioni 18. (DW Sports)

No comments:

Post a Comment