MABINGWA wa
Tanzania, Yanga imeaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kutolewa kwa
penalti 4-2 na AFC Leopards baada ya kutoka suluhu ndani ya dakika 90 katika
mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Leopards itamenyana na Gor Mahia ambayo iliifunga Nakuru All Stars mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa jioni uwanja wa Uhuru.

Mshindi katika
fainali hizo atajinyakulia dola za kimarekani 30,000 zaidi ya Sh. Milioni 65 na
nafasi ya kucheza na Everton ya England Julai 13.
Kipa namba moja wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa Marselas Ingotsi, lakini mlinda mlango wa AFC Leopards, Dennis Shika naye akacheza mikwaju ya Said Mussa na Said Juma ‘Makapu’.

Nahodha
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo mshambuliaji Mzambia, Obrey Chira ndiyo
pekee walifunga penalti za Yanga, wakati Bernard Mango, Allan Katerega, Duncan
Otieno na Dennis Shika wakafunga za AFC Leopards.
Katika dakika 90 za mchezo, timu zote zilimiliki mpira sawa, ingawa hakukuwa na mashambulizi ya kushitua.
Kikosi cha Yanga kilikuwa: Deogratius Munishi ‘Dida’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Mohammed Ally, Andrew Vincent ‘Dante’, Pato Ngonyani/Babu Ally Seif dk 61, Juma Mahadhi, Maka Edward/Said Juma dk 76, Obrey Chirwa, Yussuf Mhilu/Samuel Greyson dk 53 na Emmanuel Martin/Said Mussa dk 56.
AFC Leopards: Dennis Shika, Otieno Ian, Marcus Abwao/Mike Kibwage dk 88, Joshua Mawira, Salim Abdallah, Duncan Otieno, Mango Bernard, Allan Kateregga, Vincent Obura, Yakubu Ramadhani na Gilbert Fiamento/Marselas Ingotsi dk 56.

No comments:
Post a Comment