MCHEZO wa
kwanza wa Kundi L kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania
‘Taifa Stars’ na Lesotho ‘Mamba’ utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi kuanzia Saa 2:00 usiku.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Nchini, (TFF) Alfred Lucas alisema sababu za mchezo huo kufanyika Uwanja wa klabu ya Azam ni kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika matengenezo madogo.

Alfred amewataka
Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Azam Complex, kuisapoti timu yao ili
iweze kufanya vizuri.
Taifa Stars itaingiaa kwenye mchezo huo ikitoka kwenye kambi ya wiki moja mjini Alexandria, Misri.
Nahodha Mbwana Ally Samatta hakuwepo Misri lakini ameshaungana na wenzake Dar es Salaam akitokea Ubelgiji ambako anachezea klabu ya KRC Genk.
Kiungo wa DC Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa AFC Eskilstuna ya Denmark, Thomas Ulimwengu wao walikuwepo Misri na wako tayari kwa mchezo wa keshokutwa.

No comments:
Post a Comment