Saturday, June 10, 2017
Mashemeji Derby, Mechi ya kwanza kuchezwa ugenini Afrika Mashariki
Fainali ya michuano ya Kombe la SportPesa SuperCup inatarajiwa kufanyika kesho Uwanja wa Uhuru Dar es salaam, ikizikutanisha timu za AFC Leopards dhidi ya Gor Mahia zote kutoka Kenya.
AFC Leopards (Abhaluya) v Gor Mahia (K’ogalo) ni wapinzani wa jadi ambao licha ya wote kuwa wanatokea jiji la Nairobi, mchezo unaowakutanisha vigogo hao huitwa Mashemeji Derby.
Huu unakua ni mchezo wa kwanza kuwakutanisha watani wa jadi nje ya nchi wanayotokea, ukiwa ni mchezo wa kwanza kufanyika katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Dar es salaam, Tanzania ndipo unapofanyika mchezo huo siku ha jumapili, ambapo mshindi wa mchezo huo atacheza dhidi ya klabu ya Everton Julai 13 uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Tayari mashabiki wa Yanga wanaisapoti Gor Mahi ambayo hutumia jezi ya rangi za kijani na nyeupe, huku Simba wakiwasapoti AFC Leopards wanaotumia jezi zenye rangi nyekundu na nyeupe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment