Kituo cha
Televisheni cha Azam kimeingia makubaliano ya mwaka mmoja ya kuonesha mubashara
mashindano ya Ndondo hatua ya makundi ambayo yanachezwa katika Mkoa wa Dar es
Salaam.
Akizungumza
baada ya kutia saini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Azam TV, Tido Muhando
alisema wameamua kuingia makubaliano na Clouds Media ili kuwaonesha watu ambao
hawawezi kufika katika viwanja kushuhudia mashindano hayo.
“Tunawaahidi
Clouds na watanzania wote kuwa tutafanya kazi nzuri kwani sisi ndio kituo bora
nchini kwa urushaji wa matangazo hasa soka hilo halina ubishi,” alisema Tido.
Naye Mratibu
wa Ndondo Cup Shafii Dauda aliwashukuru Azam Media kuwa sehemu yao katika
kuendesha mashindano hayo kwa miaka minne mfufulizo.
“Lengo la
mashindano ni kutengeneza daraja kwa vijana wenye vipaji ili waonekana na
baadae wasajiliwe na timu za madaraja ya juu hivyo tunaishukuru Azam Media kuwa
sehemu yetu kufanikisha ndoto za vijana,” alisema Shafii.
Kwa upande
wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wake, Almas Kasongo
aliishukuru Azam Media na Clouds Media kwa kusaidia kuendeleza michezo Dar es
Salaam.
“Tunafurahi
kuona soka likichezwa katika mkoa wetu kwani mnasaidia kutekeleza moja ya
majukumu yetu hivyo nawaahidi mashindano haya yatasimamiwa kwa weledi mkubwa,”
alisema Kasongo.
Droo ya
makundi ya mashindano hayo inatarajiwa kuchezeshwa leo katika viwanja vya
Escape One, Kinondoni ambapo timu 32 zitakuwa kwenye bakuli moja.
Timu hizo ni
Vituka FC, Twiga International, Kigoma Kombaini, Stimtosha, Tandavamba, Black
Six, Ukwamani, Ndanda Investment, Miami, Mpakani Kombaini na Kibo Kombaini.
Vijana
rangers, Goroka FC, Burudani, Polisi DSM College, Faru jeuri, Boom FC, Temeke
Market, Temeke Squad, Tabata United, Misosi, Keko Furniture na Buguruni United.
Zingine ni
Goms United, Kigogo Kombaini, Wauza matairi, Shelaton, Makuburi, Kibada One,
Kauzu FC, Mlalakuwa Rangers na Madiba FC.
No comments:
Post a Comment