CRISTIANO Ronaldo ni noma hafai! Labda hivyo ndivyo ambavyo unaweza kumuelezea nyota huyo raia wa Ureno baada ya kuisaidia Real Madrid kutwaa taji la klabu bingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo.
Ronaldo amefunga mabao mawili kati ya manne waliyowafunga Juventus kwenye mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Millennium ambapo Mrenoowid huyo ameibuka mfungaji bora wanakwa kufikisha mabao 12.
Ronaldo aliipatia Real bao la uongozi dakika ya 20 baada ya kulmalizia kazi nzuri ya beki Dani Carvajal upande wa kulia.
Bao hilo lilidumu kwa dakika saba tu kwani mshambuliaji Mario Mandzukic aliisawazishia Juve kwa bao safi la ‘tik tak’ dakika ya 27 ndani ya eneo la 18.
Real walipata mabao mawili ya haraka dakika za 61 na 64 kupitia kwa Casemiro na Ronaldo na kuwachanganya Juve ambao mipango yao ilionekana kufeli kwa muda mrefu wa kipindi cha pili.
Kiungo Juan Cuadrado ambaye alitokea benchi alitolewa nje na kwa kadi nyekundu dakika ya 84 kufuatia kadi ya pili ya njano kwa kulipiza baada ya kuchezewa madhambi na nahodha Sergio Ramos.
Kinda Marco Asensio alihitimisha karamu ya mabao baada ya kufunga la mwisho dakika ya 90 kufuatia krosi nzuri iliyopigwa na Marcelo.
No comments:
Post a Comment