RAIS wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amesema Tanzania imejiandaa vema
kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana waliochini ya miaka 17 za
Afrika zitakazofanyika nchini 2019.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana Malinzi alisema Tanzania imeanza maandalizi kujenga
timu imara ambayo italeta ushindani kwani Serengeti boys imeonyesha njia.
“Timu
itakayoshiriki Afcon U-17 mwaka 2019 ilianza kuandaliwa tangu 2013 kwa
mashindano ya U-14 yaliyofanyika Mwanza na sasa wapo kambini Mwanza na TFF
inawagharamia kila kitu,” alisema Malinzi.
Pia Malinzi
alisema ili nchi iwe mwenyeji wa mashindano ya vijana unatakiwa kuwa na viwanja
viwili jambo ambalo Tanzania inakidhi hadi hoteli na barabara zinazounganisha
hoteli watakazofikia timu na kwenda uwanjani
“Mei 28 Rais
wa CAF ndugu Ahmad alimkabidhi Katibu
Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa uenyeji wa fainali za U-17 za mwaka 2019 tukio
ambalo lilishuhudiwa na dunia nzima,” alisema Malinzi.
Aidha
Malinzi alisema ni aibu nchi kuwa mwenyeji halafu timu ikaondolewa katika hatua
ya makundi hivyo benchi la ufundi lina kazi ya kuandaa timu imara ndio maana
wamelazimika kuwaamisha wachezaji kutoka Mwanza na kuwaleta Dar es Salaam.
Alisema
Kamati ya maandalizi ya CAF itakuja nchini kuangalia maandalizi ya viwanja vya
mashindano na mazoezi, hoteli na
barabara zitakazotumika wakati timu zikienda uwanjani.
Katika
kuthibitisha Tanzania imejiandaa kufanya maandalizi ya kutosha Malinzi alisema
watamtumia Rais wa zamani wa TFF, Leodgar Tenga ambaye amewahi kuwa mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi wa fainali za wanawake za Afrika zilizopita awape
uzoefu wa vitu vinavyoangaliwa.
Alisema
Tanzania inaweza kupata nafasi ya kucheza kombe la Dunia zijazo kwani FIFA imeongeza
wigo kwa nchi za Afrika kuwa tisa hadi 10 ikiwa ni uwiano wa timu moja katika
kila timu tano za Afrika kwani Afrika zipo 55.
No comments:
Post a Comment