Pages

Sunday, June 25, 2017

OKWI AWASILI, AGEUKA BUBU




MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Uganda, Emmanuel Okwi jana usiku aliwasili nchini na kugeuka bubu.
Okwi ambaye alipokelewa na Makamu wa Rais wa Simba Gofrey Nyange ‘Kaburu’ katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA) pia walikuwepo wandishi lakini yeye na Kaburu hawakuongea chochote.
“Nitaitisha mkutano wa wandishi wa habari mtakuja kuongea naye,” alisema Kaburu.
Alhamisi iliyopita Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa klabu ya Simba, Zacharia Hanspope alisema Okwi angewasilia Jumamosi na ndicho kilichotokea.
Okwi anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili hadi 2019 kuitumikia Simba kwa ajili ya mashindano mbalimbali kuanzia msimu ujao.
Simba itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani baada ya kutwaa taji la kombe la FA.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda “The Cranes” alijiunga na Simba mwaka 2010 akitokea SC Villa ya Uganda ambako ndiko alikoanzia soka lake la ushindani.
 Okwi aliuzwa Tunisia na kujiunga na Etoile Du Sahel ambako alijiunga na Yanga mwaka 2014, kabla ya kurejea tena Simba mwaka 2015 na kuuzwa tena nchini Denmark katika klabu ya Sonderjsky inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo na mwaka huu anarejea tena Msimbazi akitokea SC Villa ya nyumbani kwao Uganda ambayo ilimpokea baada ya kuachana na timu hiyo ya Denmark.

No comments:

Post a Comment