Pages

Friday, June 2, 2017

MALINZI: TANZANIA IPO TAYARI KWA AFCON U-17



 
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amesema Tanzania imejiandaa vema kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana waliochini ya miaka 17 za Afrika zitakazofanyika nchini 2019.
Akizungumza na wandishi wa habari jana Malinzi alisema Tanzania imeanza maandalizi kujenga timu imara ambayo italeta ushindani kwani Serengeti boys imeonyesha njia.
“Timu itakayoshiriki Afcon U-17 mwaka 2019 ilianza kuandaliwa tangu 2013 kwa mashindano ya U-14 yaliyofanyika Mwanza na sasa wapo kambini Mwanza na TFF inawagharamia kila kitu,” alisema Malinzi.
Pia Malinzi alisema ili nchi iwe mwenyeji wa mashindano ya vijana unatakiwa kuwa na viwanja viwili jambo ambalo Tanzania inakidhi hadi hoteli na barabara zinazounganisha hoteli watakazofikia timu na kwenda uwanjani
“Mei 28 Rais wa CAF ndugu Ahmad  alimkabidhi Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa uenyeji wa fainali za U-17 za mwaka 2019 tukio ambalo lilishuhudiwa na dunia nzima,” alisema Malinzi.
Aidha Malinzi alisema ni aibu nchi kuwa mwenyeji halafu timu ikaondolewa katika hatua ya makundi hivyo benchi la ufundi lina kazi ya kuandaa timu imara ndio maana wamelazimika kuwaamisha wachezaji kutoka Mwanza na kuwaleta Dar es Salaam.
Alisema Kamati ya maandalizi ya CAF itakuja nchini kuangalia maandalizi ya viwanja vya mashindano na  mazoezi, hoteli na barabara zitakazotumika wakati timu zikienda uwanjani.
Katika kuthibitisha Tanzania imejiandaa kufanya maandalizi ya kutosha Malinzi alisema watamtumia Rais wa zamani wa TFF, Leodgar Tenga ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa fainali za wanawake za Afrika zilizopita awape uzoefu wa vitu vinavyoangaliwa.
Alisema Tanzania inaweza kupata nafasi ya kucheza kombe la Dunia zijazo kwani FIFA imeongeza wigo kwa nchi za Afrika kuwa tisa hadi 10 ikiwa ni uwiano wa timu moja katika kila timu tano za Afrika kwani Afrika zipo 55.


No comments:

Post a Comment