Pages

Friday, May 5, 2017

WILDAID YAFANYA KWELI KWA SERENGETI BOYS LEO



TAASISI ya kulinda wanyama pori ya WildAid leo imekabidhi vifaa kwa Shirikisho la SokaTanzania (TFF) baada ya jana kuingia makubaliano ya kushirikiana.
Juzi Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliingia makubaliano na WildAid ya kushirikiana kupinga ujangili kupitia timu ya Taifa ya Vijana miaka 17, ‘Serengeti Boys’.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, Katibu Mkuu wa TFF,  Selestine Mwesigwa alishukuru WildAid kwa msaada huo na kusema umekuja wakati muafaka.
“Vijana wetu wetu wanaweza kuvaa fulana hizi wakati wa kupasha mwili joto katika mashindano ya Afrika pia wadau wa michezo watavaa kuonesha kuwa wanapinga ujangili,’ alisema Mwesigwa.
Naye Mshauri wa WildAid Tanzania, Lily Massa alisema wanafurahi kufanya kazi na TFF kwa sababu kupitia mchezo wa soka unapendwa na watu wengi ujumbe wao utawafikia watu wengi.
“Nafurahi kufanya kazi na TFF kwani inabeba idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja hivyo elimu kuhusu ujangili na utunzaji wa wanyama pori na mazingira itafika kwa jamii,” alisema Lily
WildAid tayari inafanya kazi na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayecheza Marekani na mwanamuziki Ali Kiba, BenPal na mfanyabiashara Mohamed Dewj ‘MO’ hivyo kuongezeka kwa TFF kunafanya wafikie watu wengi.

No comments:

Post a Comment