Pages

Friday, May 5, 2017

ABDULRAHMAN MUSSA MCHEZAJI BORA MWEZI APRILI


MCHEZAJI wa Ruvu Shooting FC, Abdulrahman Mussa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Aprili kwa msimu wa 2016/2017.
Akizungumza na wandishi wa habari Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas Abdulrahman aliwashinda wachezaji Jafar Salum wa Mtibwa Sugar  FC na Zahoro Pazi wa Mbeya City.
“Katika mwezi wa Aprili kulikuwa na raundi tatu na timu ya Ruvu Shooting ilicheza michezo miwili ambayo Abdulrahman alicheza dakika zote 180 na kufunga magoli manne,” alisema Lucas.
Pia Lucas alisema kati ya matano yaliyofungwa na Ruvu Shooting manne alifunga Abdulrahama na kuifanya timu yake kufikia nafasi ya tisa kutoka nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Abdulrahman alifunga Hat Trick katika mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Majimaji uliochezwa katika Uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Abdulrahman Mussa atazawadiwa kitita cha shilingi Milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

No comments:

Post a Comment