MALI
imefanikiwa kutetea taji lake la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri
chini ya miaka 17 baada ya kuifunga Ghana bao 1-0 katika mchezo wa fainali
uliofanyika jana usiku.
Timu hiyo
ambayo nusura isishiriki mashindano hayo kutokana tishio la kutaka kufungiwa na
Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) miezi michache iliyopita, ilidhihirisha
ubora wake kwa kuwafunika wapinzani wao hao wa Ghana.
Mamadou
Samake ndiye aliyefunga bao hilo pekee katika mchezo huo katika dakika ya 22
katika mchezo uliojaa msisimko na kushuhudia Mali ikiungana na mataifa makubwa
katika soka ya Ghana, Nigeria na Gambia kutwaa taji hilo mara mbili.
Hata hivyo,
Mali ni nchi ya kwanza kutetea taji hilo.
Black
Starlets walishindwa kuonesha kiwango chao cha awali, ambacho kiliwafanya
kufunga mabao tisa katika mechi mbili za kwanza katika mashindano hayo.
Timu hiyo
ilishindwa kabisa kufanya mashambulizi ya nguvu langoni mwa wapinzani wao.
Ghana
walikosa penalti mbili katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, ambazo
ziliokolewa na kipa wa Mali, Ibrahim Danlad.
Beki ya
Ghana ilishindwa ilishindwa kufanya maamuzi ya haraka kumzuia Danlad aliyetoa
pasi kwa Samake ambaye kwa haraka alifunga bao hilo.
John Otu na
Razak Yusif waliadhibiwa kwa mchezo mbaya adhabu zilizoshuhudia Ghana wakipewa
penalti na kushindwa kufunga.
Gabriel
Leveh alikaribi kuwasawazishia Starlets mwishoni mwa kipindi cha kwanza, lakini
kipa Youssouf Koita alidokoa mpira huo uliokuwa ukielekea langoni.
Mali katika mchezo
wa kwanza wa Kundi B ililazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya
Tanzania, Serengeti Boys, ambayo ilikuwa ikishiriki kwa mara ya kwanza
mashindano hayo.
Timu zote za
Ghana na Mali pamoja na Guinea, iliyoifunga Niger na kumaliza ya tatu,
zitaiwakilisha Afrika katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini
India Oktoba.
No comments:
Post a Comment