MADRID,
Hispania
MSHAMBULIAJI
wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amepuuza taarifa kwamba tayari amekubali
kuondoka kwenye klabu yake wakati huu wa majira ya kiangazi.
Griezmann
amehusishwa na kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi na uwezekano
huo ukichagizwa na klabu hiyo ya England kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya
kupitia ubingwa wa Europa baada ya kuifunga Ajax mabao 2-0 kwenye fainali.
Taarifa
mbalimbali zinasema makubaliano binafsi yamefikiwa kati ya mshambuliaji huyo na
Manchester United, huku ikitazamiwa atasaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo
haraka.
Mshambuliaji aliongeza uvumi wa kujiunga na klabu hiyo ya England pale
aliposema nafasi ya yeye kuelekea Manchester United ina uwiano wa sita kwa 10.
Hata hivyo
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitumia akaunti yake ya Twitter
Ijumaa hii kukanusha taarifa hizo, ingawa alikiri kuwa hatima yake bado
haieleweki.
“Uvumi wote
hauna msingi,” aliandika na kuongeza kuwa: “Bado niko Atletico Madrid. Muelekeo
wangu utajulikana baada ya mazungumzo na mshauri wangu wa michezo.”
Mapema juzi
alisisitiza kuwa anataka kushinda mataji chini ya kocha Diego Simeone.
“Umekuwa
mwaka mzuri na nina imani naweza kuwa bora zaidi na kushinda mataji na timu
hii,” alisema Griezmann na kuongeza kuwa:
“Nitafanya kila kinachowezekana. Tuna furaha
sana hapa. Tumefikia malengo yetu, labda tulihitaji zaidi, lakini
haikuwezekana.”
No comments:
Post a Comment