LONDON,
England
MKONGWE wa
soka wa England, Paul Gascoigne ‘Gazza’ ameangua kilio kutokana na hisia kali,
anapofikisha umri wa miaka 50, akisema alihisi hangefika kutokana na ulevi wa
kupindukia.
Gazza
alikutana na rafiki na wadau wake mbalimbali kwenye hafla ya kutimiza nusu
karne hiyo, ambapo pia iliendesha harambee kwa ajili ya kupambana na mzio wa
kilevi na uraibu wake.
Anasema
kufika umri huo ni hatua kubwa sana, ikizingatiwa jinsi alivyokuwa akiyachapa
maji, na kwamba sasa analenga kupambana na hali hiyo, si kwake tu, bali kwa
watu wote.
Nyota huyu
amekuwa akilinganishwa na mwingine mkubwa, George Best, ambaye kama Gazza,
alikuwa mzuri sana enzi za usakataji soka uwanjani, lakini baada ya hapo
alikuwa na kashfa za ulevi wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya kupindukia.
Katika
tawasifu yake, ‘Gazza-My Story’ Mwingereza huyo anasema kwamba tabia yake
imemtia matatani, akihangaika na maisha baada ya kumaliza uchezaji soka,
akisema kwamba mwaka jana ulikuwa mbaya zaidi katika maisha yake.
Gazza
alianzia soka yake Newcastle, akaja kuwa mmoja wa wachezaji wachache kukataa
ofa za aliyekuwa Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson, akisema sababu ni
kwamba Old Trafford ni kaskazini mno.
Mwaka 1988
aliondoka Newcastle na kujiunga na Tottenham Hotspur na pia akakipiga na Timu
ya Taifa ya England – Three Lions.
Mama yake,
Caro (72) anasema kwamba mwanawe alihamia Spurs kwa sababu ya msingi, kwamba
alikuwa amekorofishana na watu wa benchi la ufundi
la
Newcastle.
Klabu
nyingine alizochezea ni Lazio, Rangers, Middlesbrough, Everton, Burnley, Gansu
Tianmna na Boston.
Alianza
kujulikana kwa ulevi akiwa Rangers, ambapo alikuwa akiuchapa mtindi kwa sana
nyakati za usiku. Vyombo vya habari vilisimulia sana juu ya ulevi wake kuanzia
2005 baada ya yeye kuachana na soka.
Alipewa kazi
ya ukocha Kettering Town, lakini alishindwa kukaa hapo kwa muda mwngi kutokana
na tabia yake ya ulevi.
No comments:
Post a Comment