Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 11, 2013

KAMATI YA RUFAA YA UCHAGUZI YA TFF YAKESHA IKISIKILIZA PINGAMIZI ZILIZOWASILISHWA KWAO NA MAWAKILI WA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI

Mwenyekiti wa Kamati ya rufaa ya uchaguzi, Idd Mtinginjola akionyesha moja ya vielelezo vilivyowasilishwa na warufani


Mgombea Malinzi akiwa katikati ya mawakili wa upande wa utetezi na upingamizi
                                           Kamanda Mpinga na Murtaza Mangungu wakipitia vielezo
                                       Mwenyekiti Idi Mtinginjola akisoma moja ya kilelezo kilichiowasilishwa na ushahidi na Wakili wa Wambura
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi waliokuwepo kwenye kikao hicho
 Mgombea Michael Wambura akiwa na wakili wake Mpela Mpoki wakisikiliza kamati
Mawakili wakisoma magazeti ndani ya mapokezi ya ofisi ya TFF
    Wajumbe wa kamati ya uchaguzi na mgombea na wakili wake wakitoka nje kupisha kamati ya rufaa kujadiliana kuhusu uhalali wa wajumbe wa kamati ya uchaguzi kuwepo ndani ya kikao chao



Wagombea wakijadiliana na mawakili wao ndani ya ofisi za TFF eneo la mapokezi usiku wa saa tatu.

Kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF jana ilikesha ikisikiliza rufaa za wagombea zilizowasilishwa kwenye kamati.

Kikao hicho ambacho kilikuwa na uwazi wa hali ya juu kilihudhuriwa pia na waandishi wa habari lakini hawakuruhiusiwa kuuliza maswali zaidi ya wajumbe wa kamati.

Mgombea wa kwanza kusikilizwa alikuwa  Malinzi ambaye aliwasilishwa na wakili Audax Kahendaguza ambaye aliweza kupangua hoja zilizomzuia mteja wake kuenguliwa, ambapo alichukua saa tatu kuanzia saa 7.30 hadi saa 9.30.

Baada ya hapo kamati ilikwenda kupata chakula cha mchana na waliporudi aliingia wakili wa Nyamlani Peret Heller, ambaye aliweza kupangua hoja zote alizowekewa pingamizi pasi na shaka na mdau Justianian Medard ambaye alikuwa anawasilisha na wakili Moses Masiga.

Ilifika zamu wa mgombea Michael Wambura akiwakilishwa na wakili Mpale Mpoki ambaye alijitahidi kupangua hoja tatu lakini ya nne inayohusu uadilifu ilishindikana kutoka na kamati ya Mkwawa kumtia hatiani kwa kutumia madaraka yake vibaya alipokuwa Katibu Mkuu wa FAT kwa kuipata tenda kampuni yake na hakuwahi kupinga tuhuma hizo CAS kwani kamati ya Mkwawa ndio chombo cha mwisho kutoa maamuzi

Hata hivyo Wakili Mpoki alihoji uhalili wa kamati ya uchaguzi kuwepo ndani wakati ilimaliza kazi yake hali iliyosababishwa warufani, waandishi na wajumbe wa kamati ya uchaguzi kutolewa nje kwa muda baadae kurudi na kikao kuendelea.

Hata hivyo Mwenyekiti Idd Mtinginjola akiri kuwepo mapungufu kwenye kadhaa na kuaahidi kulifanyia kazi kwani haiwezekani mtu aliyekunyima haki mwanzo awepo kwenye maamuzi mengine ambayo umekatia rufaa.

Kilikuwa kikao kilichosisimua sana licha ya kuchukua muda mwingi kwani kazi ilikuwa ikifanyika kwa kunukuu katiba ya TFF, Katiba ya nchi na kanuni za uchaguzi za TFF.

Hivyo mawakili walikuwa wakitoa hoja kwa kunukuu vipengele mbalimbali kwenye katiba ya TFF, Katiba ya nchi na kanuni za uchaguzi

No comments:

Post a Comment