Pages

Monday, May 29, 2017

Conte, Wenger mambo safi



LONDON, England
WAKATI JUZI timu zao zilikuwa uwanjani kumenyana kwenye fainali ya Kombe la FA, Arsene Wenger na Antonio Conte wanasaini mikataba mipya yenye thamani ya mamilioni kwa Arsenal na Chelsea.
Wakati Wenger amekuwa akipigiwa kelele na baadhi ya wshabiki aondoke Emirates kwa kukosa ubingwa kwa muongo mzima, anapewa mkataba wa miaka miwili na kuachiwa madaraka makubwa ya kufamya uamuzi wa masuala ya soka klabuni hapo.
Kwa upande wa Conte aliyekuwa anatakiwa na klabu kadhaa kama Barcelona na nyingine Italia, anahuisha mkataba wake na atakuwa kocha anayelipwa kiasi kikubwa zaidi  cha mshahara katika historia ya klabu hiyo.
Mtaliano huyo anapewa mkataba wa pauni kadiri ya milioni 9.6 kwa mwaka na atakaa Stamford Bridge hadi 2021, miaka miwili zaidi ya wakati ambapo mkataba wa sasa unamalizika. Wakuu wameamua kumuongezea mkataba kutokana na ufanisi wake lakini pia kuzuia klabu nyingine kumchukua.

No comments:

Post a Comment