LONDON, England
WAKATI JUZI timu
zao zilikuwa uwanjani kumenyana kwenye fainali ya Kombe la FA, Arsene Wenger na
Antonio Conte wanasaini mikataba mipya yenye thamani ya mamilioni kwa Arsenal
na Chelsea.
Wakati Wenger
amekuwa akipigiwa kelele na baadhi ya wshabiki aondoke Emirates kwa kukosa
ubingwa kwa muongo mzima, anapewa mkataba wa miaka miwili na kuachiwa madaraka makubwa
ya kufamya uamuzi wa masuala ya soka klabuni hapo.
Kwa upande wa
Conte aliyekuwa anatakiwa na klabu kadhaa kama Barcelona na nyingine Italia,
anahuisha mkataba wake na atakuwa kocha anayelipwa kiasi kikubwa zaidi
cha mshahara katika historia ya klabu hiyo.
Mtaliano huyo
anapewa mkataba wa pauni kadiri ya milioni 9.6 kwa mwaka na atakaa Stamford
Bridge hadi 2021, miaka miwili zaidi ya wakati ambapo mkataba wa sasa
unamalizika. Wakuu wameamua kumuongezea mkataba kutokana na ufanisi wake lakini
pia kuzuia klabu nyingine kumchukua.
No comments:
Post a Comment