MANCHESTER,
England
BAADA ya
kuonesha umahiri golini, golikipa wa Manchester United, Sergio Romero anataka
klabu hiyo imfanye awe chaguo la kwanza hapo.
Romero
aliyechaguliwa na kufanya vyema kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Europa
anamwambia kocha wake, Jose Mourimnho asiwe na shaka hata kama kipa namba moja,
David de Gea ataondoka Old Trafford.
Ni katika msingi
huohuo, Romero anataka kuona kwamba hasajiliwi kipa nyota kutoka nje kwa ajili
ya kuwa chaguo la kwanza, bali apewe yeye, kisha madogo wachukue nafasi ya
pili,tatu na nne na wana uhakika wa kufanya vizuri.
De Gea amecheza
mechi 36 kati ya 38 za Ligi Kuu ya England, na kwa mara nyingne tena anawaniwa
na Real Madrid wanaopenda kuvunja rekodi za usajili. Madrid ndio nyumbani kwa
De Gea.
Msimu uliopita
klabu mbili hizo zilikubaliana dakika za mwisho juu ya mauzo ya mchezaji huyo,
lakini nukushi iliyotumwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ilichelewa kufika
baada ya muda wa mwisho ambao ilikuwa ni saa sita usiku. Kwa sasa Mourinho
anataka iwapo watamchukua, wawape AlvaroMorata.
No comments:
Post a Comment