*Babaye
chapombe alichoma kitanda cha mama
ARTURO
Erasmo Vidal Pardo, maarufu zaidi kwa jina la Arturo Vidal ni kiungo wa Bayern
Munich.
Alizaliwa
miaka 28 iliyopita Santiago, Chile katika lindi la umasikini, akakuzwa kwa
shida sana lakini sasa anaogelea kwenye kiasi kikubwa cha fedha.
Hapana
ubishi kwamba Vidal ni mmoja wa viungo mahiri kabisa duniani, akiwa amehudumu
kwenye klabu kubwa kama Munich, na kabla ya hapo Juventus na Bayer Leverkusen.
Aliwindwa na
Manchester United kiangazi cha mwaka jana, lakini kocha Louis van Gaal akawa na
hofu juu ya utimamu wake wa mwili na kuumia mara kwa mara. Arsenal walihusishwa
naye sana kiangazi hiki lakini amekwenda Allianz Arena.
Vidal
ameshaanza kung’aa akiwa na Bayern na kama kuna kinachoonekana ni kuhatarisha
namba ya Thomas Muller kwa sababu anaelekea kumudu zaidi na tayari ameifungia
timu yake hiyo mpya.
Wazazi wake
walikuwa watu wa hali ya chini na alikua katika hali ya ‘bora liende’ na kama
si kugundulika kwa kipaji chake cha soka, huenda leo angekuwa chokoraa.
Akiwa mtoto
alianzia timu ya Melipilla kabla ya kuingia kikosi cha vijana cha timu hiyo ya
kwao, akaonekana na Colo-Colo, klabu iliyofanikiwa zaidi Chile, akaingizwa
kwenye mfumo wao wa vijana.
Mwaka 2005
aliingizwa rasmi kwenye kikosi cha wakubwa, lakini akadumu kwa miaka miwili tu,
kwani Bayer Leverkusen walimwona na kumdaka hadi 2011 alipochukuliwa na
Juventus na mwaka huu Bayern.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Chile ameonesha kiwnago kizuri cha soka dimbani, lakini
pia utovu wa nidhamu, pengine kutokana na asili ya alikokulia au tu kwa sababu
ya ‘kunuka’ fedha ambazo pia huzichezea kwa anasa.
Akicheza
sambamba na Alexis Sanchez wa Arsenal, Vidal alifanikiwa kuwapa Chile ubingwa
kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 99, chini ya kocha Jorge Sampaoli.
Mwana huyu
mkubwa wa mama Jacqueline Pardo na baba Erasmo Vidal alipewa jina kwa heshima
ya babu yake aliyekufa ajalini wakati akiendesha gari la taka.
Nyumbani
kwao kulikuwa na usumbufu mwingi kwa sabau ya wingi wa watu, bibi aliyekuwa
hawezi tena kutembea na upungufu wa mahitaji, ikiwa ni pamoja na chakula.
Akiwa na
umri wa miaka mitano, babaye aliyekuwa chapombe alikuwa akiuza mboga katika
soko la La Vega, ambapo baada ya kuupiga mtindi alitia moto kitanda cha mama
yao.
Baba huyo
alifukuzwa na baadaye Vidal akatokea kuwa kama baba wa nyumba, huku mama yake
mzazi akifanya kazi ya usafi kwa watu.
Tangu akiwa
na umri wa miaka tisa, Vidal alikuwa akikwepa shule na baada ya utoro wake huo
alikuwa akinyomga baiskeli yake kwa maili sita hadi Santiago kulikokuwapo na
mbio za farasi.
Alikuwa na
kazi kubwa ya kuwalisha na kuwapanga inavyotakiwa kutoka kwenye mashikizo yao,
lakini huku akiwa makini kuchunga kiasi kidogo cha fedha alichokuwa akikusanya
ili kisije kuibwa au kupotea.
Alishiriki
pia katika kamari kwamba ni farasi yupi angeshinda mbio hizo; akipata ushauri
wa mkubwa mmoja kumsaidia kuweka dau la nani angeshinda wakati familia na
rafiki zake walimsubiri katika Jumuiya ya San Joaquin.
Binafsi
alipenda kushiriki mbio za farasi lakini alikuwa na wasiwasi iwapo angeweza;
hivyo aliendelea na kazi ya kuwatunza.
Hata hivyo,
bosi wake, Enrique Carreno, alipata kumwona akicheza na mpira pembezoni siku
moja na alimwambia hivi juu ya farasi na mbio zake.
“We mwana,
mchezo huu wa farasi haukufai, maisha yako ya baadaye ni kwenye soka,”
alimwambia na tangu hapo Vidal akaongeza mazoezi.
Alipofikisha
umri wa miaka 15, Vidal alimwahidi mamaye kwamba angekuja kumfanya kuwa malkia
na kwamba hangefanya tena kazi za hovyo wala kuishi maisha ya shida.
Na kweli,
maneno yake yalikuja kutimia alipoingia kwenye soka, akamjengea nyumba nzuri na
zaidi ya hapo alikuwa na hamu ya kusoma, akaenda masomoni.
Moja ya tatuu
zake ipo moja ya mbio za farasi, nyingine yenye sura ya mama yake iliyo chini
kidogo ya bega lake la kulia.
“Mama
alifanya kazi ngumu sana. Huwa namsaidia kwa kila ninaloweza na najihisi
kuwajibika pia kwa wadogo zangu. Nilianza zamani sana kazi ya ‘ulezi’ kwa
sababu nilikuwa kama baba nikiwa bado mtoto na napenda sana kuhusishwa na hali
hiyo,” anasema Vidal.
Baba yake
alijaribu kujiua mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na 2008 baada ya kuchapa mtindi
aina ya Pisco ambayo ni wiski.
Miaka mitatu
baadaye alikamatwa sambamba na dada yake wakidaiwa kujihisisha na usafirishaji
mihadarati baada ya polisi kumkamata akiuza kokeini.
Baba mkubwa
wa Vidal aitwaye Ricardo ambaye hakuwa na makazi zaidi ya kuishi mitaani kwenye
viambaza vya majumba ya watu alikuwa mlevi wa kupindukia na alifariki dunia
miaka miwili iliyopita.
Wakati
akiitunza familia yake ndipo bosi wake kwenye mbio za farasi akagundua kipaji
chake cha soka na akawa anacheza mchangani karibu na klabu ya Kanisa Katoliki
ya Rodelindo.
“Daima
ungemwona akiwa na mpira wa miguu, aliupenda sana, alilala nao, akaamka nao,
akacheza kabla na baada ya shule, aliporudi nyumbani kwa chakula cha mchana na
baada ya kuacha shule,” anasema mjomba wake, Victor.
Vidal
alikuja kupachikwa jina la utani la 'Cometierra' ambalo maana yake ni ‘mla
vumbi’ kutokana na jinsi alivyochafuka kila mahali kwa vumbo kwa sababu ya
mchezo wake na hadi leo ameshikilia mtindo huo wa kucheza.
“Tulijua
angekuja kuwa mchezaji mzuri sana, tulimuunga mkono kwa hilo na sasa tunafurahia,”
anasema kiongozi wa klabu hiyo ya Kanisa na rafiki wa familia yake, Ramon
Henriquez.
“Alipenda
kusema kwamba anataka kwenda kuionesha dunia uwezo wake na kwamba angekuwa
mchezaji wa kulipwa. Na kweli, amekuja kucheza na magwiji kama Gianluigi Buffon
na Andrea Pirlo,” anasema.
No comments:
Post a Comment