Mwamuzi Isihaka Mwalile akisaidiwa na Hellen Mduma pamoja na Rashid Zongo waliutendea haki mtanange huo na kuwafanya wachezaji, viongozi na mashabiki waliohudhuria kukubali matokeo bila kinyongo chochote
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amewataka waamuzi wengine kufuata sheria za soka ili bingwa apatikane kwa haki na kupunguza malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali.
“Hawa ni waamuzi wa walioonyesha uwezo mkubwa wa kuchezesha soka, wao na sheria, sheria na wao! Mambo mengine hawana. Wamependwa na kila mtu uwanjani kwa kuchezesha kwa haki vyombo vyenye mamlaka watumieni vizuri ni wazuri sana,” alisema Masau.
Masau alisema mchezo huo ulitawaliwa na vionjo, ufundi na burudani ya kutosha kutokana na timu zote kucheza soka lenye kuvutia bila kukamiana wala kuumizana.
Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Abdulrahman Mussa dakika ya 61 kwa mkwaju wa penati baada ya kipa wa City Fikirini Bakari kucheza rafu eneo la hatari huku Zahoro Pazi akisawazisha dakika ya 63.
City inayofundishwa na kocha Mmalawi Patrick Phiri, wamefikisha pointi 31 wakiwa nafasi ya sita wakati Ruvu ya kocha Hamsini Malale wakikusanya pointi 29 na kushika nafasi ya tisa.
No comments:
Post a Comment