Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 7, 2015

YANGA KWENDA MBEYA KESHO, WAKATI AZAM FC WAO WAKO ZANZIBAR




YANGA inatarajia kuondoka kesho alfajiri kwenda Mbeya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa ngao ya jamii, huku wapinzani wao, Azam FC nao wakijichimbia visiwani Zanzibar.
Akizungumza baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe alisema wanaondoka na wachezaji wote ambao wamesajiliwa msimu huu.
“Tutaondoka alfajiri na tutakwenda kuweka kambi Tukuyu lakini tutakwenda Mbozi kucheza na Kimondo FC ambayo inacheza daraja la kwanza na tutacheza na timu ya Zesco ya Zambia na Butter Bullet ya Malawi kwenye Uwanja wa Sokoine”, alisema Hafidh
Azam FC na Yanga watamenyana  Agosti 22, mwaka huu katika mchezo wa Ngao, kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza Septemba 22.
Mechi  hii inatarajiwa kuwa ya kukata na shoka kutokana na upinzani wa Azam FC na Yanga katika miaka ya karibuni, zikiwa ndizo timu ambazo zinapokezana ubingwa wa Ligi.
Ikumbukwe mara ya mwisho zilipokutana katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Kagame timu hizo zilimaliza dakika 90 bila kufungana kabla ya Azam FC kushinda kwa penalti 5-3 hivyo kwenye mechi ya ngao ya jamii iwapo timu hizo hazitafungana ndani ya dakika 90, mikwaju ya penalti itaamua mshindi. 

No comments:

Post a Comment