Kamati
ya Rufani za Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetupa
rufaa Saleh Saleh maarufu kama Ndonga aliyelalamikia kuhusu uamuzi wa Kamati ya
Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kadhalika
kumlalamikia Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Almas Kasongo akitaka ang’olewe
kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa sasa.
Pia katika uamuzi wake huo Kamati ya
Rufaa za Uchaguzi ya TFF, imesema kila upande ubebe gharama zake kwani rufaa
hyo haina sababu za msingi za kusitisha mchakato wa usaili au kuweza kumuengua
Kasongo katika kinyang’anyiro cha kugombea uongozi DRFA.
Saleh Ndonga alikata rufaa dhidi ya
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) -
Mrufaniwa wa Kwanza - na Mwenyekiti wa sasa wa DRFA, Almas Kasongo –Mrufaniwa
wa Pili akitaka jina lake liondolewe katika orodha ya wagombea wa nafasi ya
uenyekiti wa DRFA.
Pingamizi lake liliegemea kwenye
sababu kuu mbili ambazo ni mosi, ni kwamba Kasongo hakuwa na sifa za kuwania
tena nafasi hiyo ya mwenyekiti wa DRFA kwa kile alichodai kukosa sifa za
uadilifu, uaminifu kadhalika ni mvunjaji wa katiba kwa mujibu wa katiba ya
DRFA. Pia alidai kuwa alishindwa kuitisha mkutano mkuu kwa muda unaotakiwa.
Pingamizi hilo awali liliondolewa na
Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na hivyo akakosa imani za kamati hiyo na kwenda
kwenye Kamati ya Rufaa za Uchaguzi. Alidai kwamba Kamati ya Uchaguzi ya DRFA
ilikosea kikatiba kuondoa pingamizi bila kujali hoja za msingi kikatiba
zilizokuwamo kwenye pingamizi lake.
Hivyo Ndonga mbele ya kamati ya
rufani za uchaguzi inayoongozwa na Dk. M. Lugaziya alitaka chombo hicho cha TFF
kufuta uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, iondoe jina la Kasongo na asiweze
kugombea nafasi ya uongozi wa mpira popote Tanzania; arudishe gharama za
pingamizi na aamuriwe kurejesha gharama nyingine zozote ambazo kamati inaona
inafaa azilipe.
Mrufaniwa Kasongo alipinga rufaa
hizo kwa maelezo ya jumla kuwa uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA ulikuwa
sahihi na rufaa iliyoletwa rufani iliyoletwa na Ndonga haina mashiko hivyo
akaomba itupiliwe mbali.
Kasongo alieleza kuwa kinachoelezwa
kuwa ni hesabu zingeweza kuletwa kwenye mkutano wa Uchaguzi ambao ufanyike Februari,
lakini umesogezwa mbele hadi Aprili 9, mwaka huu na kamati iliona kuwa
kuchelewa kwa taarifa ya hesabu zilizokaguliwa katika mazingira haya hakuwezi
kuchukuliwa kama ni kilelelezo cha kukosa uadilifu au uaminifu. Hiyo
inaweza kuwa ni hukumu ya mapema mno.
Kuhusu kushindwa kuitisha mkutano,
mrufaniwa Kasongo alitetea kuwa aliitisha kwa mujibu wa katiba isipokuwa
kulikuwa na kipindi ambacho Ndonga na baadhi ya viongozi wa Chama Cha mpira wa
Miguu cha Temeke (TEFA) walifungiwa kabla ya busara zake na Rais wa TFF, Jamal
Malinzi kuwarejesha madarakani kutokana na mzozo iliyodhirisha kulikuwa na uasi
uliosababisha kufungiwa.
Kamati imejiridhisha kwamba kwa
mujibu wa Katiba Ndonga na wenzake walikuwa na nafasi ya kuomba mkutano wa
dharura, jambo ambalo hakuna ushahidi kama wamewahi kufanya hivyo baada ya
kurejea madarakani bada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya uasi.
Kamati imezitaka kamati zote za
uchaguzi wanachama wa TFF kama vile mikoa na klabu, kufanya kazi zao kwa
weledi.
No comments:
Post a Comment