TFF YATOA RAMBIRAMBI KIFO CHA MKURUGENZI WAO WA FEDHA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa
Mkurugenzi wake wa Fedha na Utawala, marehemu Edgar Masoud. Edgar Masoud aliyefariki dunia jana
jioni Machi 27, 2017 aliugua ghafla juzi Jumapili akiwa kanisani kabla
ya kukimbizwa Hospitali ya Bochi iliyoko Mbezi kwa Msuguri ambako
alikutwa na mauti akipatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment