WACHEZAJI wa
timu ya Taifa ya soka ya Vijana waliochini ya miaka 17, ‘Serengeti boys’
wamekabidhiwa bima za Afya na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF)
Akizungumza
wakati ya hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NHIF, Kurasini Dar es Salaam,
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano,
Angela Mziray alisema afya ni mtaji wa kwanza kwa mtu hivyo wameamua
kuwekeza kwa wachezaji wa Serengeti boys kwa vile wanaitangaza vema Tanzania.
“Serengeti
boys wameitangaza vema Tanzania na sisi tukaona tutumie fursa hii kujitangaza
kwa sababu wanatuwakilisha kimataifa hivyo tunawakabidhi Toto Afya kadi kila
mmoja, “ alisema Angela.
Pia Angela
alisema si mara yao ya kwanza kufanya kazi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kwani tayari ni wadhamini wenza kwenye ligi kuu.
Naye Katibu
Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa aliishukuru NHIF kwa kuwapatia bima wachezaji
hao kwani TFF ilikuwa inatumia pesa nyingi kuwahudumia pindi wanapougua au
kupata majeraha wakiwa kambini.
“Naipongeza
NHIF kwa kuwapatia bima wachezaji wa Serengeti boys na nawapomba msiishie
kwenye timu hii tu bali na timu nyingine za taifa na klabu,” alisema Mwesigwa.
Toto Afya
kadi ni bima kwa watoto wenye umri wa kuanzia siku moja hadi miaka 18 na
huchangiwa sh. 50,600 kwa mwaka.
NHIF imefika
asilimia 90 nchi nzima wakiwa na vituo zaidi ya 6000 kwa ajili ya kutoa huduma ya bima ya afya.
No comments:
Post a Comment