Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 24, 2017

MTIHANI WA KWANZA WA MAYANGA KESHO UWANJA WA TAIFA



TIMU ya Taifa ya soka ‘Taifa Stars’ kesho inashuka Uwanjani kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana utakaofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ni kipimo cha kwanza kwa kocha Salum Mayanga unasubiriwa kwa hamu kupima uwezo wake kwani safari hii amerudi kama kocha Mkuu baada ya kuwa kwenye benchi la timu hiyo akiwa kocha msaidizi enzi za kocha Mdenmark Mart Nooij
Akizungumza na wandishi wa habari leo alisema anatarajia kuutumia  mchezo huo kujua mapungufu ya kufanyia kazi kabla ya kuingia kwenye mechi za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani
“Ni michezo muhimu na tunatarajia itatupa mwanga mzuri wa maandalizi kabla ya mechi za kufuzu AFCON na CHAN,”alisema Mayanga
Pia Mayanga alisema anafurahi kuwasili kwa mchezaji Farid Mussa ambaye aliwasili usiku wa kuamkia jana na kusema atamtumia katika mchezo huo huku akisikitika kumkosa Thomas Ulimwengu ambaye ni majeruhi
Naye kocha wa Botswana, Petter Buffer, raia wa Uingereza alisema amekuja na kikosi kizuri kikiongozwa na nahodha wao Ofendse Nato anayecheza India na anatarajia matokeo mazuri.
Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alisema wako vizuri na tayari kwa ajili ya mchezo huo huku akitarajia utakuwa mgumu kwa sababu wanacheza na timu ya taifa ambao wamejipanga pia
“Kwa sababu tutakuwa nyumbani, tunatarajiwa matokeo mazuri kwani kikosi chetu kina mchanganyiko mzuri wa wachezaji ambao ni wazoefu na wasio na uzoefu hivyo tuunge mkono mabadiliko yaliyofanywa na kocha kwani wachezaji wazoefu tulitumika kwa muda mrefu bila mafanikio,” alisema Samatta.
Baada ya mchezo wa leo Taifa Stars itakuwa na mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Burundi ambao utachezwa keshokutwa kwenye uwana huo wa Taifa ambao utahusisha wachezaji wanaocheza ligi ya ndani pekee.
Taifa Stars itaanza kuwania tiketi ya CHAN mwaka ni nchini Kenya kwa kucheza na Rwanda mechi ya kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Julai 14 na 16 kabla ya timu hizo kurudiana Uwanja wa Amahoro, Kigali kati ya Julai 21 na 23.
Ikifanikiwa kuitoa Rwanda, Tanzania itamenyana na mshindi kati ya Uganda na ama Sudan Kusini au Somalia katika Raundi ya Tatu ya mchujo mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Agosti 11, 12 na 13 na marudiano kati ya Agosti 18, 19 na 20, mwaka huu
Tanzania imewahi kushiriki mara moja tu fainali za CHAN, ambayo ilikuwa ni mwaka 2009 zikifanyika kwa mara ya kwanza kabia nchini Ivory Coast nakutolewa katika hatua ya makundi.
Kwa upande wa AFCON, Taifa Stars imepangwa Kundi L pamoja na Uganda, Cape Verde na Lesotho.
Mshindi wa kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON ya 2019, wakati timu nyingine tatu zitakazomaliza nafasi ya pili na wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama washindi wa pili bora.
Tanzania imewahi kucheza mara moja tu fainaliza AFCON, mwaka 1980 nchini Nigeria ambako ilitolewa hatua ya makundi pia. 

No comments:

Post a Comment