Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi nne kabla ya Jumapili Februari 12,
mwaka huu kuendelea kwa michezo mitatu katika viwanja mbalimbali hapa
nchini.
Stand United inatarajiwa kuwa mwenyeji wa
Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga wakati
Simba itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam huku Ndanda ikiialika Toto Africans kwenye Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, kadhalika Ruvu shooting ikichea na Azam FC kwenye Uwanja wa
Mabatini, Pwani.
Jumapili, Mwadui FC itacheza Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui
wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam ilihali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwenye Uwanja wa
Mkwakwani mjini Tanga. Kwa ufupi, ratiba ya kesho iko kama ifuatavyo:
11.02.2017 - STAND UNITED VS MAJIMAJI
11.02.2017 - SIMBA VS TANZANIA PRISONS
11.02.2017 - NDANDA FC VS TOTO AFRICAN
11.02.2017 - RUVU SHOOTING VS AZAM FC
12.02.2017 - MWADUI VS MBEYA CITY
12.02.2017 - AFRICAN LYON VS MTIBWA SUGAR
12.02.2017 - JKT RUVU VS MBAO FC
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Kundi A mechi zinatarajiwa
kupigwa leo Februari 10, mwaka huu ambako Lipuli itaikaribisha Ashanti
United kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa wakati Pamba itacheza na
Mshikamano ilihali Friends rangers itacheza na Kilivya United wakati
Polisi Dar itapambana na Africans Sports.
10.02.2017 - LIPULI VS ASHANTI
10.02.2017 - PAMBA VS MSHIKAMANO
10.02.2017 - FRIENDS RANGERS VS KILUVYA
10.02.2017 - POLISI DAR VS AFRICAN SPORTS
Kundi B
Kundi B kesho Jumamosi Februari 11, mwaka huu itacheza na Mlale JKT
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Njombe Mji itacheza na
Coastal Union kwenye Uwanja wa Makambako mkoani Njombe.
11.02.2017 - MLALE JKT VS KURUGENZI FC
11.02.2017 - NJOMBE MJI VS COASTAL UNION
Kundi C
Kundi C kutakuwa na mechi nne ambako Mgambo Shooting itacheza na
Polisi Dodoma wakati Polisi Mara itakuwa mwenyeji wa Mvuvumwa ya Kigoma
wakati Rhino Rangers itakuwa mgeni wa Panone huko Kilimanjrao na Singida
United itacheza na Alliance mjini Singida.
11.02.2017 - MGAMBO SHOOTING VS POLISI DODOMA
11.02.2017 - POLISI MARA VS MVUVUMWA
11.02.2017 - PANONE VS RHINO RANGERS
11.02.2017 - SINGIDA UNITED VS ALLIANCE SCHOOL
Ligi Daraja la Pili leo Februari 10, kutakuwa na mchezo mmoja wa
Kundi A kati ya Mirambo ya Tabora na Bulyanhulu ya Shinyanga wakati
Jumapili Februari 12, mwaka huu kutakuwa na mechi tatu ambazo ni za
Kundi D.
Mechi nyingine ni kati ya Namungo na Mawenzi; Sabasaba na The Mighty
Elephant wakati Mkamba Rangers itacheza na Mbalali United.
10.02.2017 - MIRAMBO VS BULYANHULU
12.02.2017 - NAMUNGO VS MAWENZI
12.02.2017 - SABASABA VS THE MIGHTY ELEPHANT
12.02.2017 - MKAMBA RANGERS VS MBARALI UNITED
No comments:
Post a Comment