| ||||
Meneja Uhusiano wa TTCL,
Nicodemus Mushi (wa pili kushoto mbele) akizungumza kwa niamba ya Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba kwenye hafla ya
uzinduzi wa mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach
Soccer' yaliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ufukwe wa Coco Beach na
kushirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia
ni Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam wa Kampuni ya TTCL, Jane
Mwakalebela akiwa katika uzinduzihuo.
|
Mkuu wa Biashara Kanda
ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane
Mwakalebela (katikati) akimkabidhi kiasi cha fedha shilingi laki nne
(400,000/-) pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa
simu na intaneti (5GB) kwa muda wa mwezi mmoja nahodha wa timu ya Chuo
cha Ardhi (kulia) baada ya kuibuka washindi wa pili wa Mashindano ya
Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo
mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Nchini (TFF). Mashindano hayo yalifanyika Ufukwe wa Coco
Beach jana. Kulia ni Bw. Dimo Dibwe muandaaji wa mashindano hayo.
|
Baadhi ya waamuzi wa Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakijadiliana jambo kabla ya mechi kuendelea. |
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea. |
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea. |
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea. |
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea. |
Wakati mashindano hayo
yakiendelea wanafunzi wa vyuo waliendelea kujishindia zawadi mbalimbali.
Kushoto ni Ofisa Masoko wa TTCL, Eric Muganda akimkabidhi vocha ya muda
wa maongezi wa thamani ya shs10,000/- baada kushinda moja ya michezo
iliyoambatana na zawadi kwa wanafunzi waliokuwa wakishiriki mashindano
ya soka la ufukweni.
|
Baadhi ya timu zilizoshiriki Mashindano ya vyuo Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' zikishangilia baada ya kushinda mechi za awali. |
Mbwembwe za mabingwa...! Mabingwa wa Mashindano ya Vyuo Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' wakiwa katika moja ya pozi mara baada ya kutangazwa kuwa mabingwa. |
Kikosi cha Timu ya Chuo cha Ardhi ambao waliibuka washindi wa pili katika Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TTCL ambao ni wadhamini wa mashindano hayo. |
No comments:
Post a Comment