YANGA leo
wamefanya mazoezi ya jasho na damu kwa muda wa saa moja kujiandaa na mchezo wa
ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam
Katika
mazoezi hayo ambayo kitaalumu yanaitwa saketi wachezaji walionekana kuchoka
lakini walifanya hadi mwisho na kuhitimisha na kucheza mpira kwa dakika 30
Saketi ni
muunganiko wa mazoezi mengi kwa pamoja sehemu nyingine yanahusisha mpira na
sehemu nyingine bila mpira kwa mazoezi hayo mchezaji anapata stamina, unyumbufu
na uvumilivu vitu ambavyo ni muhimu kwenye mechi.
Akizungumza
baada ya mazoezi, kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alisema ni maandalizi
ya mchezo dhidi ya African Lyon utakaochezwa kesho kwenye uwanja huo.
“Maandalizi
ni mazuri na wachezaji wana ari na kwenye mazoezi umeona wamefanya vizuri japo
yalikuwa na ugumu lakini kwa ujumla tupo vizuri,” alisema Mwambusi
Pia Mwambusi
alisema kipa Beno Kakolanya ndie pekee aliye majeruhi kwani anasumbuliwa na
nyonga
Naye nahodha
msaidizi, Haruna Niyonzima alikiri kwenye ligi hakuna timu ndogo hivyo
wanachukulia uzito mchezo huo na kisaikolojia wapo vizuri kwa sababu wamelipwa
stahili zao.
“Unapoona
wachezaji wanafanya mazoezi ina maana wamelipwa haki zao hivyo kazi yetu ni
kuhakikisha mchezo na African Lyon tunashinda ili tuwape mashabiki wetu zawadi
ya krismasi,” alisema Niyonzima
Habari za
ndani zinasema wachezaji hao wamelipwa posho za mchezo wao na JKT Ruvu huku
wakiahidiwa kulipwa mshahara muda wowote kabla ya Ijumaa.
Yanga ambayo ina pointi 36 kwenye nafasi ya pili inacheza na African Lyon
inayoshika nafasi ya 12 ikiwa na ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza michezo 16
kila moja.
No comments:
Post a Comment