SIMBA, YANGA NA AZAM FC KUENDELEZA UBABE MAPINDUZI?
UHONDO wa soka sasa
unahamia visiwani Zanzibar ambapo vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga
zitapambana kuwania ubingwa wa Kombe la Mapinduzi lililoanza kutimua vumbi jana
kwa timu ya Taifa Jang'ombe dhidi ya ndugu zao, Jang'ombe Boys.
Hata hivyo, ukiachana na mechi hiyo, kitimutimu
kitaanza rasmi kesho kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi, URA ya Uganda dhidi ya KVZ kuanzia saa 10:00 jioni kabla ya
Simba kumenyana na Taifa ya Jang'ombe saa 2:30 usiku.
Mechi za Kundi B zitaanza Jumatatu kwa Azam FC kumenyana na Zimamoto kuanzia saa
10:00 jioni kabla ya Yanga kumenyana na Jamhuri saa 2:30 usiku.
Yanga itashuka dimbani bila ya beki wake raia wa
Togo, Vincent Bossou ambaye ana majukumu ya timu yake ya taifa iliyo kwenye maandalizi ya mwisho ya
kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayotarajiwa kuanza
Januari 14 nchini Gabon ambapo Togo
ilikata tiketi ya kushiriki michuano
hiyo baada ya kuinyuka Djibouti mabao 5-
0.
Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa Yanga, Baraka
Deusdetit, kikosi hicho cha Yanga kitaondoka alasiri leo kikiwa na wachezaji 26
na benchi zima la ufundi baada ya mazoezi yao ya mwisho asubuhi watakayofanya
kwenye uwanja wa Uhuru.
Kikosi kamili cha Yanga kinachokwenda Zanzibar
ni makipa: Deogratius Munishi 'Dida', Benno Kakolanya na Ali Mustafa 'Barthez'.
Mabeki ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Pato
Ngonyani, Vincent Andrew, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kelvin Yondan, Juma Abdul
na Oscar Joshua.
Viungo ni Haruna Niyonzima, Justin Zulu, Simoni
Msuva, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashiuya, Deus Kaseke, Saidi Juma 'Makapu',
Thabani Kamusoko na Yussuf Mhilu.
Washambuliaji ni Donald Ngoma, Amisi Tambwe,
Emmanuel Martin, Obrey Chirwa na Matheo Anthony.
Kwa upande wa Simba wanaondoka kikosi kizima
kikiongozwa na nahodha Jonas Mkude, mlinda mlango Daniel Agyei, Javier Bukungu,
Mohamed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto,
Muzamiru Yassin, James Kotei, Pastory Athanas, Mohamed Ibrahim, Peter Manyika,
Hamad Juma, Novatus Lufunga, Juma Luizio, Said Ndemla, Moses Kitandu na Laudit
Mavugo.
Simba pia itamkosa beki wake Juuko Murshid
ambaye pia yupo kwenye kikosi cha Uganda kinachokwenda Ufaransa kujiandaa na
michuano ya Afcon.
Wakati Azam ambayo itaanza harakati zake kesho,
itaondoka leo pia na itamenyana na Zimamoto katika mchezo utakaofanyika saa 10
alasiri kesho.
Yanga imepangwa kundi B katika michuano hiyo ya kila mwaka ikiwa na Azam FC ya Dar es Salaam, Jamhuri na Zimamoto
zote za Zanzibar.
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika
Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia jana Desemba hadi Januari 13, Kundi A lina
timu za Simba, Taifa ya Jang’ombe, Jang’ombe Boys, KVZ na mabingwa watetezi,
URA ya Uganda.
Simba, Yanga na Azam zinakwenda kwenye michuano
hiyo zikiwa kwenye tatu bora katika msimamo wa Ligi Kuu bara ambapo Simba
inaongoza kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Yanga yenye pointi 40 na Azam ina
pointi 30.
No comments:
Post a Comment