KOCHA wa
timu ya Simba ya U-20, Nico Kiondo amesema haikuwa kazi rahisi kuchukua ubingwa
wa Ligi ya Viajana wa timu za U-20 yaliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Chamazi
Dar es Salaam
Akizungumza
na gazeti hili Kiondo ambaye timu yake imeifunga Azam FC kwa penalti 5-3 baada
ya dakika 120 kumalizika kwa sare mabao 2-2 alisema Ligi ilikuwa ngumu kwani
timu zote zilikuwa na wachezaji wazuri.
“Namshukuru
Mungu pia wachezaji wangu kwani walijituma na kuhakikisha wanachukua ubingwa,
wanastahili pongezi kwa sababu walijitoa na kupigana kufa na kupona,” alisema
Kiondo
Katika
mchezo huo ambao ulihudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
timu zote zilionyesha kandanda safi na lililojaa ufundi.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14 lililofungwa na Moses Kitandu akimalizia pasi ya George Emmanuel, lakini Shaaban Iddi akaisawazishia Azam FC dakika ya 28.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14 lililofungwa na Moses Kitandu akimalizia pasi ya George Emmanuel, lakini Shaaban Iddi akaisawazishia Azam FC dakika ya 28.
Dakika ya
57, Said Mohammed akaifungia Azam FC bao lakini Said Hamisi kuisawazishia Simba
dakika ya 83 na kufanya dakika 90 zimalizike kwa sare 2-2 hivyo kulingana na
kanuni ikabidi ziongozwe dakika 30.
Katika
dakika 30 za nyongeza ili kukamilisha dakika 120 hakuna timu iliyoweza kuongeza
bao hivyo walilazimika kwenda kwenye penalti ili mshindi apatikane.
Penalti za
Simba zilifungwa na Calvin Faru, Said Hamisi, Mokiwa Perus, Vincent Costa na
Moses Kitandu, wakati za Azam zilifungwa na Abbas Kapombe, Rajab Mohammed na Adolph
Bitegeko huku ya Said Mohamed ikipanguliwa na kipa wa Simba, Ally Salum.
Katika
mchezo wa nusu fainali, Simba iliitoa Stand United kwa penalti 8-7 baada ya
sare ya 1-1 wakati Azam iliitoa Mtibwa Sugar kwa penalti, 4-2 kufuatia sare ya
bila kufungana ndani ya dakika 120.Hii ni ligi ya kwanza ya vijana kuchezwa hapa hapa nchini ikishirikisha timu 16 zilizoanzia kwenye hatua ya makundi katika Kituo cha Kagera na Dar es Salaam.
Ligi hii inamalizika huku ikiacha kumbukumbu ya kuhuzunisha kufuatia kifo cha mchezaji wa Mbao FC, Ismail Mrisho Khalfan, wakati timu yake ikicheza na Mwadui FC baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui.
Ismail (19) alifariki Desemba 4, Bukoba baada ya kuanguka uwanjani dakika ya 74 Uwanja wa Kaitaba, dakika chache baada ya kuifungia bao timu yake katika ushindi wa 2-0 na akazikwa nyumbani kwao Mwanza siku iliyofuata.
No comments:
Post a Comment