![](https://static.standard.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2016/01/05/10/JoseMourinhoOT.jpg)
Mourinho, ambae ametua Man United mwanzoni mwa Msimu huu, alianza vizuri kwenye EPL, Ligi Kuu England, lakini baadae wakayumba na sasa wamerudi kwenye reli na wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 3 nyuma ya timu ya 5 Tootenham, pointi 4 nyuma ya Arsenal walio nafasi ya 4,pPointi 6 nyuma ya City ambao ni wa 3, pointi 7 nyuma yaw a 2 Liverool na 13 nyuma ya vinara Chelsea.
Akiongea na Wanahabari kuelekea Mechi yao ya Jumatatu na Sunderland, Mourinho amesema: “Watu wanataka kuwa na furaha tena…Watu wana matumaini makubwa ingawa kwa sasa hatupo nafasi nzuri!”
Mourinho, ambae sasa ameiongoza Man United kwenye mechi 10 bila kufungwa, ametoboa kuwa hajawahi kuongea na Moyes.
Mourinho pia aliponda Ratiba ya EPL kwa kipindi hiki cha Krismasi na Mwaka Mpya na kudai baadhi ya Klabu zimependelewa.
Ameeleza: “Kipindi hiki kigumu cha Mechi mfululizo, Chelsea wako na ratiba nyepesi isiyokuwa msongamano. Sie tofauti lakini tumezoea kwani tuko Europa Ligi!”
No comments:
Post a Comment