MSHAMBULIAJI wa Azam
FC, John Bocco amefurahia ushindi wa bao 1-0 walioupata juzi dhidi ya Prisons
katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Akizungumza na gazeti hili jana Bocco alisema ni
faraja kwao na uongozi kwani michezo miwili mfululizo walipata sare kiasi
kwamba timu ilishuka kutoka kwenye nafasi ya tatu hadi ya tano lakini
anashukuru wamerejea juu tena.
“Timu yetu ni nzuri lakini matokeo ya uwanjani
yamekuwa siyo ya kuridhisha sana hivyo ushindi wa bao 1-0 unaleta faraja japo
tunatakiwa kupambana ili tuwe bingwa,” alisema Bocco.
Pia Bocco alisema wanakwenda kwenye kombe la
Mapinduzi na wanatarajia kurudi na kombe.
Azam watafungua dimba na Zimamoto mchezo
utakaochezwa saa kumi alasiri leo kwenye Uwanja wa Amaan.
Azam ambayo ilicheza bila kocha wake Zeben
Hernandes aliyefutwa kazi, ilipata bao lake katika dakika ya 40 ya mchezo huo
likifungwa na nahodha Bocco kwa shuti kali.
Ushindi huo umeirudisha Azam nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 30 sawa
na Kagera Sugar wakiwazidi kwa uwiano wa mabao.
Simba inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi
44 huku Yanga ikishika nafasi ya pili na pointi 40.
No comments:
Post a Comment