UONGOZI wa Yanga
umekubali kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi kwenye mechi yao na
Simba endapo Shirikisho la Soka nchini (TFF) litakubali.
Hivi karibuni Msemaji wa Simba, Haji Manara aliweka wazi kuwa hawataingiza timu uwanjani dhidi ya Yanga endapo mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini kwa madai kuwa hawatendewi haki.
Hivi karibuni Msemaji wa Simba, Haji Manara aliweka wazi kuwa hawataingiza timu uwanjani dhidi ya Yanga endapo mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini kwa madai kuwa hawatendewi haki.
Hata hivyo
jana TFF, kupitia kwa Ofisa habari wake, Alfred Lucas, lilisema kanuni za ligi
hazijakataza waamuzi kutoka nje ya Tanzania bali suala hilo linahitaji mjadala
wa kina baina ya pande zote.
Makamu Mwenyekiti
wa Yanga, Clement Sanga, amesema kuwa kama TFF itakubali ombi la Simba mechi
yao kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya Tanzania hawatakuwa na pingamizi ila
ametoa angalizo kuwa tukio hilo litashusha hadhi ya waamuzi nchini.
"TFF
wakikubali tukicheza na Simba mchezo uchezeshwe na waamuzi kutoka nje hatuna
shida ila wanatakiwa kulitazama kwa umakini suala hili kwakuwa linaweza kuleta
mpasuko kwenye soka letu," alisema Sanga.
Sanga alisema waamuzi wanafanya kazi kubwa za kutafsiri sheria 17 za soka na pia sio kazi rahisi kama watu wanavyochukulia hivyo TFF inatakiwa kufanya maamuzi sahihi kwa mustakabali wa soka letu na waamuzi.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuingia kambini Jumatatu tayari kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi.

No comments:
Post a Comment