MWAKILISHI
wa Tanzania katika shindano la Miss Afrika 2016, Julitha Kabete, kesho
atapanda jukwaani moja na washiriki wenzake 18 kuwania taji la mrembo wa
michuano hiyo linalofanyika nchini Nigeria.
Mashindano
haya yatakayofanyika nchini Nigeria, jimbo la Cross River, Calabar , mshindi wa
kwanza katika shindano hilo atajipatia kitita cha dola za Kimarekani 25,000,
sawa na Sh.milioni 52 ya Tanzania pamoja
na gari jipya.
Mshindi
wa pili katika shindano hilo atapata kitita cha dola ya Kimarekani 15,000
sawa na Sh.milioni 33 za Kitanzania na wa tatu dola 10,000 sawa na Sh.milioni 22.
Akizungumza
na Gazeti hili, mshiriki huyo alisema kikubwa anaomba Watanzania wamuombea dua
haweze kushinda taji hilo.
Kabete
alisema kuna upinzani mkali, lakini nae kwa upande wake anajiamini anauwezo
mkubwa wa kufanya vizuri na kubeba taji la shindano hilo.
"Nina
nafasi ya kufanya vizuri, kikubwa naomba dua zetu Watanzania wenzangu, niweze
kufaya vizuri na kubeba taji,"alisema Kabete.
Mrembo huo
ameenda kushiriki shindano hilo alikiwa chini ya kampuni ya Millen Magese
Group (MMG), inayomilikiwa na Happiness 'Millen' Magese, anayefanya
shughuli zake za mitindo nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment