Pages

Saturday, November 5, 2016

MSUVA MCHEZAJI BORA OCTOBA



MSHAMBULIAJI wa Yanga,  Simon Msuva amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas alisema Msuva amewashinda wachezaji Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin.
"Msuva alikuwa na washindani wa karibu wawili katika kinyang'anyiro hicho cha Oktoba kutoka Simba, ambao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin na kuwashind", alisema Lucas.
Kwa mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14  baada ya kufunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho.
Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Msimu uliopita Msuva aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom na ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza na Zimbabwe Novemba 13.

No comments:

Post a Comment