Pages

Tuesday, October 4, 2016

REFA AKIRI KOSA KUMPA BALOTELLI KADI NYEKUNDU


JANA Mario Balotelli alipiga Bao la Pili na la ushindi kwa Timu yake Nice ya France katika Dakika ya 86 walipoifunga Lorient 2-1 lakini Dakika chache baadae Refa Olivier Thual alimlamba Mchezaji huyo Kadi za Njano 2 na kumtoa kwa Kadi Nyekundu.
Lakini, baada ya kuitazama tena Mechi hiyo kwenye TV, Refa Thual alikiri kukosea kumpa Kadi ya Njano ya Pili Balotelli na sasa huenda Mchezaji huyo kutoka Italy akafutiwa Kifungo.
ua Nice kwa Mkopo Siku ya Mwisho ya Dirisha la Uhamisho hapo Agosti 31 akitokea Liverpool ambako ameonekana hafai, amekuwa akiwika huko France kwa kuifungia Nice Bao 6 katika Mechi 5 na kuiweka kileleni mwa Ligi 1.
Hapo Jana, Balotelli alipewa Kadi ya Njano ya Kwanza baada ya kuvua Jezi akisherehekea Bao lake la ushindi na Dakika chache baadae akakwaruzana na Mchezaji wa Lorient Stevem Moreira bila kutokea rabsha yeyote lakini Refa Thual akawapa wote Kadi za Njano na kumtoa nje Balotelli kwa Kadi Nyekundu.
Hii Leo, Mkuu wa Ufundi wa Marefa huko France, Pascal Garibian, ameliambia Jarida la L'Equipe kwamba Refa Olivier Thual amerudia kuitazama Mechi hiyo na amekiri alikosea kutoa Kadi ya Njano ya Pili kwa Balotelli na yupo tayari kutoa ushahidi huo mbele ya Kamati ya Nidhamu itakayopitia Kesi ya Balotelli.

Inatarajiwa Kamati hiyo itaketi Alhamisi na kumsafisha Balotelli kuendelea kuichezea Nice baada ya Mapumziko ya Ligi 1 ya Wiki 2 kupisha Mechi za Kimataifa.
Balotelli hakuitwa na Kocha Giampiero Ventura kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Italy ambacho Alhamisi kitacheza na Spain kwenye Mechi ya Kundi lao kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

No comments:

Post a Comment