KESHO
patachimbika Anfield, ambapo watani wa jadi wa kihistoria nchini England,
Liverpool na Manchester United watakabiliana kwenye mechi ya Ligi Kuu ya
England (EPL).
Ni wakali
wawili – Jurgen Klopp na Jose Mourinho wanaokutana, huku Klopp wa Liverpool
akiwa na nafuu zaidi kwa jinsi mwelekeo wa ligi unavyoendelea.
Wakati
Liverpool hadi Jumamosi asubuhi walikuwa wamekaa katika nafasi ya nne wakiwa na
pointi 16, Man U walikuwa katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 13 na
wachezaji wa Man U wamekuwa wakilaumiwa kwa kucheza chini ya kiwango, huku
kukiwa na tetesi za kutaka kuuzwa kwa nahodha wao, Wayne Rooney.
Mechi hii ya
mahasimu ambayo huku Uingereza hujulikana kama ‘derby’ na mahsusi kwa hii
ni ‘North-West Derby’ kwa maana ya kwamba ni mechi ya watani wa jadi walio
kwenye ukanda wa Kaskazini Magharibi ya England.
Hawa wawili
katika historia ya England ndio watani wa jadi kama ilivyo Tanzania kwa Yanga
na Simba.
Hii ni mechi
kubwa zaidi ya kihasimu kuliko hata kwa dhidi ya Everton ambao wapo jirani
zaidi na Liverpool au hata baina ya Manchester United na Manchester City walio
kwenye mji mmoja.
Uhasama huu
umechangiwa, pamoja na mambo mengine, miji mikubwa wanakotoka timu hizi, kwani
ndiyo majiji makubwa ya hapa England – Liverpool na Manchester yakitanguliwa na
London.
Kadhalika
historia ya uchumi wao na mchuano wa kiviwanda unachangia kwa kiasi kikubwa
kuupa utamu utani wao huu.
Hizi ni timu
kubwa kwa hakika, zikiwa zimepata heshima ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja
na kupata ubingwa nyumbani na Ulaya na kuwa na washabiki wengi hata ng’ambo,
Ukiwachanganya
kwa pamoja wamepata kutwaa makombe 38 ya ligi hapa nyumbani, manane ya Ulaya,
matatu ya Uefa, moja la Kombe la Dunia la Klabu, moja la Intercontinental Cup
na 36 ya FA kwa Ngao ya Jamii.
Timu hizi
kijiografia zipo umbali wa maili 35 na tangu wakati ule wa mapinduzi ya viwanda
pamekuwapo msuguano na utani baina yao kuhusiana na masuala ua uchumi na
viwanda, kila mji ukijidai kwamba upo juu ya mwingine.
Katika karne
ya 18 Manchester ilikuwa juu zaidi na kuonekana kama ndiyo kioo cha ukanda wa
Kaskazini lakini Liverpool hawakuwa wakipenda hilo.
Kwa upande
mwingine ni kwanba Liverpool ilikua moja ya miji mikubwa ya bandari huku kukiwa
na ukuaji wa masuala ya viwanda vya nguo.
Kutokea kwa
Vita ya I ya Dunia kulivuruga soka ya hapa nyumbani, ambapo mashindano yalianza
tena 1919 ambapo Liverpool walikuwa juu huku United wakishuka na kuja kushushwa
daraja 1923 na kuwa huko chini kwa misimu mitatu.
Wakati Man U
wakipata uthabiti mwaka 1947, Liverpool walishuka daraja huku United wakiwa
chini ya nahodha wa zamani wa Liverpoo, Matt Busby, na kutwaa Kombe la FA 1948.
Baadaye
walikuja kutwaa makombe matatu ya Ngao ya Hisani. Ni hapo Mwenyekiti wa
Liverpool, Tom Williams alimfuata Bill Shankly na kumuuliza ni utayari gani
aliokuwa nao kwa ajili ya kuifundisha ‘klabu kubwa zaidi England?” yaani
Liverpool, naye akamuuliza “Kwa nini? Matt Busby anaondoka?”
Kweli
aliondoka na Shankly akachukua mikoba akawapandisha daraja Liverpool
kuwarudisha juu walikokuwa.
Kesho
wanakutana wakiwa na makocha tofauti, Liverpool wakiwa na kocha mpya kwa msimu
wa pili sasa, akiwa ametoka Borussia Dortmund wakati Man United wanaye kocha
mpya kwa msimu wa kwanza, akiwa alifukuzwa Chelsea kwa kufanya vibaya mno msimu
uliopita.
Wote ni
watambaji lakini Klopp anajulikana kwa kuwajenga vyema Liver huku Mourinho
akianza vyema ligi lakini wachezaji wake bado wanamchanganya, ama hajaweza
kuwapa mfumo mzuri au kuwapanga ipasavyo kwenye namba husika.
No comments:
Post a Comment