Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL)
inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mitatu
ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye
Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam JKT Ruvu yenyewe itaialika Mtibwa Sugar kwenye
Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza, kundi A
kutakuwa na mchezo kati ya Pamba ya Mwanza na Polisi Dar kwenye CCM
Kirumba wakati African Sports itakuwa mwenyeji wa Kiluvya United kwenye
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo ya Daraja la Kwanza itaendelea Jumapili Oktoba 9, 2016 kwa
mchezo utakaozikutanisha Ashanti United na Friends Rangers; zote za Dar
es Salaam. Kadhalika Jumatatu, kutakuwa na mchezo kati ya Mshikamano ya
Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa. Mchezo huo, pia utafanyika Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.
Kundi B leo kutakuwa na mchezo kati ya
Kurugenzi ya Iringa na Coastal Union ya Tanga ufakaofanyika huko Mufindi
ukifuatiwa na michezo mitatu siku ya Jumapili Oktoba 9 ambayo Mlale
itacheza na Polisi Moro huko Uwanja wa Majimaji, mjini Songea wakati
Njombe Mji itaikaribisha Kemondo wakati KMC itacheza na Mbeya Warriors
kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Kundi C leo Mvuvumwa ya Kigoma itacheza na Singida United ya Singida wakati
Panoni itapambana na Alliance huku Polisi Dodoma itacheza na Polisi Mara
wakati Jumapili Rhino ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT ya
Tanga.
No comments:
Post a Comment