Akiongea
mbele ya waandishi wa Habari leo hii, Kiganja amesema kwamba hatua hiyo
iliyofanywa na viongozi wa Yanga chini ya mwenyekiti wa klabu Yusuphu
Manji imeenda kinyume na katiba ya klabu.
"Taarifa
nilizonazo sheria ya muungano ya wadhamini sura ya 318 ya mwaka 2002
imeeleza wazi vilabu hivi vina bodi ya wadhamini lakini wametuelekeza
sisi kwamba pamoja na kukutajia majina lakini wametueleza kua bodi ya
wadhamini wa klabu ya Yanga ni bodi ya mpito ambayo wanataka kuifuta
sasa bodi ya mpito haiwezi kufanya maamuzi makubwa ambayo watanzania
zaidi ya milioni tatu waamuliwe na watu ambao hawajapata ridhaa ya
wanachama"alisema Kiganja.
Kiganja
amesema kwamba klabu hiyo kwa sasa haina baraza hai la wadhamini kwani
muda wao umeshaisha hivyo anashangaa kuona baraza hilo linachukua jukumu
la kuikodisha timu ikiwa wao wenyewe kwa sasa hawana sifa za kuwa
wadhamini wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment