Pages

Wednesday, October 19, 2016

LIGI DARAJA LA PILI KUANZA OCTOBA 29



LIGI daraja la pili inatarajiwa kuanza Octoba 29 na kushirikisha timu 24 ambazo zimegawanywa katika makundi manne.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Alfred Lucas, alisema raundi ya kwanza itamalizika Desemba 18 na raundi ya pili itaanza Desemba 31 na kumalizika  Februari 5.
" Ligi hii imepangwa kulingana na eneo au sehemu timu zinapotoka ili kupunguzia timu gharama", alisema Lucas
Pia Lucas alisema kundi A lina timu za Bulyankulu ya Shiyanga, Green Warriors ya Pwani , Mirambo ya Tabora, Mji Mkuu ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na Mashujaa ya Kigoma
Kundi B lina timu za AFC, JKT Oljoro, Madini FC na Pepsi zote za Arusha, African Wanderers ya Iringa na Kitayosa FC ya Kilimanjaro
Kundi C linaundwa na timu za Abajalo FC, cHANGANYIKE fc, Cosmopolitan FC na Villa Squad zotw za Dar es Salaam, Bukinafaso ya Morogoro na Kariakoo ya Lindi
Kundi D lina timu za Mawenzi FC, Mkamba Rangers na Sabasaba FC za Morogoro, Mbarali United ya Mbeya, Namungo FC ya Lindi na The Might  Elephant ya Ruvuma.
Wakati huo huo Lucas amewataka viongozi wa timu za daraja la kwanza kuhakikisha wanachukua kadi za usajili za wachezaji wao kwani kuanzia mzunguko wa tano hakuna mchezaji ambaye ataruhusiwa kucheza bila kuwa na kadi halisi ya usajili wa msimu huu.


No comments:

Post a Comment