Pages

Saturday, October 1, 2016

KICHUYA ATIBUA SHEREHE JANGWANI BAADA YA KUSAWAZISHA BAO







Simba na Yanga zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi kuu uliotawaliwa na vurugu kubwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ilianza taratibu huku timu zote zikisomana lakini dakika ya 13 Thaban Kamusoko alipata nafasi ya kuifungia Yanga bao la uongozi lakini mpira wake wa kichwa ulipaa juu ya lango kufuatia krosi ya beki Haji Mwinyi.

Amisi Tambwe aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 26 baada ya mabeki wa Simba kuweka mtego wa kuotea ambapo aliwazidi akili na kumfunga golikipa Vicent Agban kirahisi.

Mwamuzi Martin Saanya alimwonyesha kadi nyekundu nahodha wa Simba Jonas Mkude baada ya kumkwatua kwa kupinga uamuzi wa refa kukubali bao alililofunga na Amis Tambwe kwa madai alikuwa ameshika kabla ya kufunga bao hilo.
Licha ya kuwa pungufu Simba waliendelea kumiliki mpira ambapo kiungo Mwinyi Kazimoto aliweza kuwadhibiti Yanga hasa katika eneo la katikati ya uwanja ambapo aliweza kuvuruga mipango yote ya mabingwa watetezi hao.

Dakika ya 86 Shiza Kichuya aliisawazishia Simba bao baada ya kupigwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango Barthez akiwa hana la kufanya.

Yanga iliwatoa Yondani, Juma Mahadhi na Deus Kaseke na kuwaingiza Andrew Vicent,Simon Msuva pamoja Haruna Niyonzima huku Simba ikiwapumzisha Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo na Lufunga na kuwaingiza Juuko Murshid,Mohamed Ibrahim pamoja na Frederick Blagnon

No comments:

Post a Comment